Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maadhimio ya Bunge yatokanayo na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika kikao kilichofanyika Dodoma Januari 19,2024.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa maadhimio ya Bunge yatokanayo na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kilichofanyika Dodoma Januari 19,2024. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw.Dustan Shimbo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia), Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Dustan Shimbo wakiwa katika kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa maadhimio ya Bunge yatokanayo na taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji ya maadhimio ya Bunge yatokanayo na taarifa ya kamati hiyo, kilichofanyika Dodoma Januari 19,2024.Katiba na Sheria, kilichofanyika Dodoma Januari 19,2024.

Kaimu Mkurugezi wa Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Hanifa Selengu akiwa katika kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa maadhimio ya Bunge yatokanayo na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kilichofanyika Dodoma Januari 19,2024.

============================================================================

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kushughulikia hoja za Muungano kupitia vikao vya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) hoja 22 kati ya 25 za Muungano zimepatiwa ufumbuzi.

Mhe. Hamza amesema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maadhimio ya Bunge yatokanayo na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika kikao kilichofanyika Dodoma Januari 19, 2024.

Amesema Ofisi inafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo na maamuzi ya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano na kufanya ziara za ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi za Muungano kwa pande zote mbili.

“Ofisi imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu na faida za Muungano ikiwemo hatua zilizochukuliwa kutatua hoja za Muungano. Elimu hiyo imetolewa kupia machapisho mbalimbali, vyombo vya habari, makongamano, maonyesho ya shughuli mbalimbali za kitaifa, majarida na vipeperushi.

“Serikali imekuwa ikifanyia kazi makubaliano ambayo yamefikiwa katika utatuzi wa hoja kwa kufanya ziara za ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya Taasisi za Muungano kwa pande zote mbili za Muungano,” amesema Mhe. Khamis.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *