Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu maswali bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge jijini Dodoma leo Januari 31, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Januari 31, 2024 kuhusu mkakati wa Serikali wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi, katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijadiliana jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge

jijini Dodoma leo Januari 31, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwasili bungeni jijini Dodoma kushiriki kipindi cha maswali na majibu katika Kikao cha pili Mkutano wa 14 wa Bunge leo Januari 31, 2024.

============================================================================

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wizara za kisekta imeanza kufanya tathmini nchi nzima kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho kukabiliana na athari za kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa aliyetaka kujua lini Serikali itafanya utafiti kuyabaini maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Katika kushughulikia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali imeanza kuyafanyia kazi maeneo hayo kwa kutekeleza miradi ya mazingira pande zote mbili za Muungano.

Amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa tuta linalozuia maji ya bahari kuingia kwenye makazi na mashamba unaotekelezwa eneo la eneo la Sipwese Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini, Pemba.

Halikadhalika, amesema mradi huo unatekelezwa pia katika eneo la Mikindani, Mtwara ambako kunajengwa ukuta utakaosaidia kupunguza kasi ya maji ya bahari kuingia kwenye makazi ya watu na kuta kwa ajili ya kurejesha fukwe katika hali yake.

Awali, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamisalisema Serikali inaendelea na kampeni za kuhamasisha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo zoezi la upandaji wa miti katika maeneo yote nchini.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Mariam Nasoro Kisangi aliyeuliza mkakati ya Serikali wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi, Mhe. Khamis alisema Ofisi ya Makamu wa Rais inafanya kampeni hizo kwa kushirikiana na taasisi kuhamasisha ubunifu, utafiti na uendelezaji wa teknolojia za kukabiliana na changamoto hiyo.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *