Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji wa Kikafu – Bomang’ombe uliopo katika Kijiji cha Kwasadala Wilaya ya Hai akiwa ziarani Mkoani Kilimanjaro tarehe 20 Machi 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika eneo la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga kwaajili ya kutembelea na kukagua chanzo cha maji cha mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mkurugenzi msaidizi wa Usanifu na Usimamizi wa Miradi ya Maji Wizara ya Maji Mhandisi Abbas Muslim wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Maji na Wakandarasi kuhusu kukamilisha kwa wakati mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024.

default
default
default
Baadhi ya picha zinazoonesha maendeleo ya mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe.

============================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameagiza uongozi wa Wizara ya Maji pamoja na watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha miji ya Same na Mwanga inapatiwa huduma ya maji safi na salama kupitia mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe ifikapo mwezi juni mwaka huu 2024.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo kilichopo eneo la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Amewataka watendaji wa Wizara ya Maji kujipanga vizuri kuwasimamia wakandarasi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili adhma na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa juu ya mradi huo yaweze kutekelezwa.

Makamu wa Rais amesema wananchi wa maeneo hayo wamesubiri mradi huo kwa miaka 19 tangu ulipoahidiwa mara ya kwanza hivyo ni wakati wa kuhakikisha mradi huo unakamilika. Amemtaka Waziri wa Maji kutembelea mradi huo mara kwa mara ili kutambua changamoto na kuzitatua haraka iwezekanavyo.

Aidha Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanalinda mazingira na chanzo cha maji ya mradi huo ili kuwa endelevu.

Wakandarasi wa Mradi huo wameahidi kufikia malengo yaliyowekwa ya kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo mwezi juni mwaka huu 2024.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *