Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme akiwasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Machi 18, 2024 kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakimkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme aliyewasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Machi 18, 2024 kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais ikiongozwa na Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma na kujitambulisha leo Machi 18, 2024.

=========================================================================

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amewasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kuanza kutekeleza majukumu yake, leo Machi 18, 2024.

Mara baada ya kuwasili katika viwanja vya vya Ofisi hiyo, Bi. Mndeme amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na kutambulishwa kwa watumishi na kuwasalimu.

Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwa Menejimenti na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, Naibu Katibu Mkuu Mndeme amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo.

Bi. Mndeme ameahidi kutoa ushirikiano kwa watendaji hao na kuomba ushirikiano kutoka kwao ili kutekeleza majukumu ya Ofisi hususan katika eneo la Mazingira alilokabidhiwa.  

Itakumbukwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alimuapisha Naibu Katibu Mkuu Mndeme Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 13, 2024 akichukua nafasi ya Dkt. Switbert Mkama aliyestaafu utumishi wa umma.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *