Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa ufafanuzi kuhusu Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma leo Machi 21, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa ufafanuzi kuhusu Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma leo Machi 21, 2024.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kuwasilisha na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma leo Machi 20, 2024. 

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christine Mndeme akijitambulisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kuwasilisha na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma leo Machi 20, 2024. 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha kuwasilisha na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma leo Machi 20, 2024. 

Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao cha kuwasilisha na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma leo Machi 20, 2024. 

===========================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafoamesema Serikali itaendelea kufanya vikao vya kujadili Masuala ya Muungano ili uendelee kuwa imara kwa maslahi ya wananchi.

Amesema hayo wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma leo Machi 21, 2024.

Pamoja na hatua hiyo pia, Mhe. Dkt. Jafo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya Muungano ili kuwajengea wananchi uelewa.

Katika kuadhmisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 2024, Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali itatoa elimu kupitia kitabu kinachotarajia kuzinduliwa wakati wa maadhmisho hayo.

Kwa upande mwingine amesema kuwa Ofisi inatarajia kukamilisha na kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu na Mkakati wa utekelezaji wake ambao utaimarisha uchumi na hifadhi ya mazingira. 

Aidha, katika taarifa hiyo iliyowasilishwa kwenye kamati imeelezea kuhusu Serikali kusimamia usawa wa mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Jimbo kwa kuzingatia Sheria ya Mfuko wa Jimbo ambayo inatumika Tanzania Bara na Zanzibar.

Sanjari na hilo imeelezwa kuwa vigezo viliyowekwa katika Sheria hiyo ni asilimia 25 ya fedha hugawanywa sawa kwa idadi ya majimbo yote.

Asilimia 10 ya fedha za Mfuko wa Jimbo hugawanywa kulingana na ukubwa wa eneo wakati asilimia 20 hugawanywa kulingana na kiwango cha umaskini.

Mfuko wa Jimbo wenye lengo la kuchochea maendeleo ya majimbo ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, asilimia 45 hugawanywa kulingana na idadi ya watu. 

Aidha, amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa ushauri walioutoa kwa Ofisi ya Makamu wa Rais ambao umesaidia katika mafanikio na kuahidi kuendelea utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Florent Kyombo ameahidi kamati hiyo itaendelea kuisimamia vyema Ofisi ya Makamu wa Rais ili malengo mahsusi ya kazi yatimie.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *