Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli inatekeleza agizo la Serikali la upandaji miti milioni 1.5 kila mwaka ambapo hadi kufikia Machi 2024 zaidi ya miti laki tano imepandwa.

Mkuu wa Idara ya Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Bw. Amir Mulsary amesema miti hiyo hupandwa na wananchi kwa kushirikiana na Serikali kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo katika taasisi, mashamba, milima na kandokando ya barabara.

Amesema lengo la upandaji miti ni utunzaji wa mazingira, upatikanaji endelevu wa maji kwa ajili ya shughuli mbalimbali za binadamu, Wanyama na viumbe hai wengine.

“Halmashauri ina hifadhi za misitu zenye ukubwa wa zaidi ya milioni 13 sawa na asilimia 17 ya eneo la halmashauri.”

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge Kitaifa 2024 inasema “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.”

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *