Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizojitokeza wakati wa michango mara baada ya kuwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma leo Aprili 23, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akichangia mara baada ya wabunge kuchangia hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 jijini Dodoma leo Aprili 23, 2024.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Naibu wake Mhe. Khamis Hamza Khamis mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka fedha 2024/25 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 23, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Naibu wake Mhe. Khamis Hamza Khamis wakipongezwa na mawaziri pamoja na wabunge mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka fedha 2024/25 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 23, 2024.

============================================================================

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kiasi cha shilingi bilioni 62.7 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 23, 2024.

Hotuba ya bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ilichangiwa na wabunge mbalimbali ambao baadhi yao wamepongeza jitihada za Serikali za kutatua hoja za Muungano na namna inavyoshughulikia hifadhi ya mazingira.

Awali akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizojitokeza wakati wa majadiliano, Waziri Dkt. Selemani Jafo amelihakikishia Bunge kuwa hoja nne zipo katika hatua za utatuzi.

Amesema faida za Muungano ni nyingi zikiwemo mahusiano mazuri kati ya wananchi wa pande zote mbili na hivyo kufanya biashara pamoja na kujenga uchumi.

Kwa upande wa mazingira Dkt. Jafo amesema kutokana na biashara ya kaboni kushika kasi Serikali imeamua kujenga uwezo kwa wataalamu wa mazingira katika Serikali za Mitaa ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu.

Hata hivyo, amesema athari za mabadiliko ya tabianchi ni kubwa na kutokana na hali hiyo Serikali inaendeleza jitihada za kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa. 

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na MazingiraO Mhe. Khamis Hamza Khamis akichangia hoja amesema elimu ya Muungano itaendelea kutolewa ili wananchi wapate uwelewa Zaidi na kuuenzi Muungano.

Amesema elimu ya Muungano inatolewa wakati wowote kupitia makongomano mbalimbali huku akiongeza kuwa kutokana na umuhimu huo Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa kitabu kitakachoelimisha wananchio kuhusu Muuungano wakati wote.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *