Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi wa Ofisi hiyo, Bi. Arafa Mkubwa muda mfupi aada ya kuwasili katika ofisi hiyo, mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake Aprili 8, 2024.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Hassan Mitawi (katikati) akimwonesha jambo Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme  muda mfupi baada ya Mhandisi Luhemeja  kuwasili katika ofisi hiyo, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja akisalimiana na watumishi wa ofisi hiyo, muda mfupi aada ya baada ya kuwasili katika ofisi hiyo, mji wa serikali, mtuma jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake aprili 8, 2024.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo akiwa ofisini kwake na viongozi waandamizi wa ofisi hiyo, kushoto Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme muda mfupi baada ya aada ya kuwasili katika ofisi hiyo, mji wa serikali, Mtumba Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake Aprili 8, 2024.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya aada ya kuwasili katika ofisi hiyo, Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake Aprili 8, 2024.

============================================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypran Luhemeja amesema ipo haja ya Ofisi hiyo kuandaa mkakati wa ubunifu wa kuutangaza Muungano na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu hifadhi endelevu ya mazingira.

Ametoa rai hiyo wakati wa kikao baina yake na Viongozi na Watendaji Waandamizi wa Ofisi hiyo kilichofanyika muda mfupi baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kuanza kutekeleza majukumu yake ya kazi Aprili 8, 2024.

Mhandisi Luhemeja amesema Muungano ni tunu muhimu kwa Watanzania na hivyo ipo haja ya wananchi kufahamu vyema historia yao na kutokana na umuhimu huo, mikakati mahsusi haina budi kuwekwa ili kuhakikisha makundi yote katika jamii yanafahamu na kuelewa Misingi, Chimbuko na Historia ya Muungano.

“Kuna Wizara 26 ndani ya Serikali, lakini jukumu la kutangaza Muungano tumepewa Ofisi ya Makamu wa Rais hususani katika kipindi hiki ambacho Muungano wetu unafikisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwake, tunapaswa kuwa na mikakati ya ubunifu iliyo endelevu katika kutoa elimu kwa umma” amesema Mhandisi Luhemeja.

Kwa mujibu wa Mhandisi Luhemeja, mkakati huo ujumuishe utoaji wa elimu kupitia makongamano na midahalo mbalimbali itakayojenga taswria chanya kwa Watanzania kuweza kufahamu fursa na manufaa ya muungano kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.

Kuhusu hifadhi na usimamizi mazingira, Mhandisi Luhemeja amesema mafanikio makubwa yameendelea kupatikana hata hivyo juhudi na msukumo mkubwa zaidi unahitajika katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira ikiwemo suala la upandaji miti.

“Tunapaswa sasa kuja na mkakati mahsusi wa kuhakikisha jamii inajenga utamaduni wa kuhakikisha kila mtu anapanda pale anapokata mti kwani kwa kufanya hivi kutasaidia kukabiliana na madhara ya uharibifu wa mazingira” amesema Mhandisi Luhemeja.

Akifafanua zaidi Mhandisi Luhemeja amewataka viongozi na watendaji hao kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kujiwekea malengo na vipaumbele vinavyoweza kupimwa na kutekelezeka.

kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi na watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware.

Itakumbukwa kuwa kabla ya kuhamia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Luhemeja alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na walemavu).

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *