Maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wanaoshiriki Mbionza Mwenge wa Uhuru 2024 wakiongozwa na Afisa Misitu Mwandamizi Bw. Thimotheo Mande wametoa elimu ya mazingira wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kirinjiko iliyoko Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Bw. Mande amesema lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi hao ni kuwafanya waone suala la utunzaji wa mazingira lipo mikononi mwao tangu wakiwa na umri mdogo ili wanapokuwa wakubwa wanufaike na miti wanayoipanda ya kivuli na matunda.

Tangu kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa mkoani Kilimanjaro Aprili 2,2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wameweza kupita katika halmashauri saba za mkoa wa Kilimanjaro na kutoa elimu kwa wananchi.

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge Kitaifa 2024 inasema “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.”

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *