Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango wakati wa dua ya pamoja ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 52 ya kifo chake tarehe 07 Aprili 2024 iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 52 ya kifo chake tarehe 07 Aprili 2024 iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, viongozi mbalimbali pamoja na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakiomba dua mbele ya kaburi la Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 52 ya kifo chake tarehe 07 Aprili 2024 iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiondoka katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi -Kisiwandui Zanzibar mahali lilipo kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume mara baada ya kuhitimishwa dua ya pamoja ya kumuombea Hayati Karume katika kumbukizi ya miaka 52 ya kifo chake tarehe 07 Aprili 2024.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *