Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na viongozi, watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 8, 2024. Wa tatu kushoto ni katiu mkuu wa ofisi ya makamu wa rais, mhandisi Cyprian Luhemeja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisalimiana na Viongozi na Watendaji Ofisi ya Makamu wa Rais baada ya kuwasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa Serikali, Mtuma jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na viongozi, watendaji na watumishi wa ofisi hiyo Aprili 8, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu Mhandisi Cyprian luhemeja (katikati) baada ya kuwasili katika Ofisi hizo zilizopo Mji wa serikali, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na viongozi, watendaji na watumishi wa ofisi hiyo aprili 8, 2024. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na viongozi, watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 8, 2024 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na viongozi, watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo aprili 8, 2024.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na viongozi, watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 8, 2024 jijini Dodoma.

Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia hotua ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati wa mkutano wake na viongozi, watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 8, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati), Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa tatu kushoto) na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano na viongozi, watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo Aprili 8, 2024 jijini Dodoma.

=============================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amehimiza umoja, amani, upendo na mshikamano kwa Watumishi wa Ofisi hiyo ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo na kuchochea kasi ya kuimarika kwa Muungano na hifadhi endelevu ya Mazingira.

Amesema hayo wakati wa mkutano wake na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika hafla ya ukaribisho wa Katibu Mkuu, Mhandisi Cyprian Luhemeja aliyewasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma kuanza kutekeleza majukumu yake ya kazi Aprili 8, 2024.

Waziri Jafo amesema rasilimaliwatu imara katika wizara, idara na taasisi ya umma inajengwa na misingi ya umoja, amani, upendo na mshikamano na iwapo misingi hiyo itazingatiwa Ofisi husika itapiga hatua kuwa ya maendeleo huku akitolea mfano Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo katika kipindi cha miaka mitatu imepata mafanikio makuwa katika kuimarisha Muungano na hifadhi endelevu ya Mazingira.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ofisi ya Makamu wa Rais imepata mafanikio makuwa katika masuala ya Muungano na Mazingira, ambapo jumla ya Hoja 15 za Muungano zimepatiwa ufumbuzi na katika eneo la Mazingira Ofisi hiyo kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuongezewa fedha za kutekeleza miradi malimali.   

“Mwezi machi mwaka huu nimetimiza miaka mitatu katika Ofisi hii na kwa pamoja tumeleta mafanikio makubwa na yanayoendelea kuleta sifa na heshima kwa kiongozi wetu mkuu Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango amaye ana majukumu ya kikatia ya kuwa mshauri wa kwanza wa mhe. Rais lakini pia kusimamia masuala ya Muungano na hifadhi ya Mazingira,” amesema Dkt. Jafo.

Aidha, amemtaka Mhandisi Luhemeja kushirikiana kwa karibu na watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo kwani wengi wao wana uzoefu, weledi, nidhamu na maarifa ya hali ya juu katika utendaji kazi na hivyo kuweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake.

Amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa idii, nidhamu na maarifa kwani kwa upande wao kama viongozi wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaendelea kuimarisha mazingira ora ya kazi pamoja na kuoresha maslahi malimali ya watumishi.

Pia, amewataka wakuu wa idara na vitengo pamoja watendaji na watumishi ndani ya ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa pamoja, kuimarisha ushirikiano na mahusiano ili kuhakikisha mafanikio makuwa zaidi yanaendelea kupatikana na hivyo kuendelea kuleta sifa kwa viongozi wa ofisi hiyo.

Kwa upande wake, Mhandisi Luhemeja alimshukuru Waziri Jafo kwa maelekezo aliyotoa kwa watendaji na watumishi wa ofisi hiyo na hivyo kuahidi kuyafanyia kazi kwani dhamira ya serikali ni kuhakikisha watumishi wa umma wanaendelea kufanya kazi katika mazingira ora na wezeshi.

“Nakushuru mhe. Waziri kwa maelekezo uliyotupatia sisi watendaji na watumishi sote tunaahidi kuyafanyia kazi ili kuhakikisha tunasukuma mrele gurudumu la maendeleo ya ofisi hii amayo ina jukumu kuwa katika kuimarisha Muungano na hifadhi endelevu ya Mazingira” amesema mhandisi luhemeja.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi na Watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware.

Itakumbukwa kuwa kabla ya kuhamia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Luhemeja alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).

     

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

-->